Mar 7, 2015

MATAJIRI YANGA SC 'WAWATIA MIZUKA' WACHEZAJI WAUE MNYAMA JUMAPILI TAIFA

Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha Yanga kimeendelea kujifua kwa mazoezi makali kabla ya kuwavaa watani wao Simba lakini jana jioni kikapokea ugeni ambao ukaachia mshiko wa maji.
Yanga ambayo imeweka kambi Bagamoyo katika hoteli ya Kiromo huku wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Chuo cha Uvuvi Mbegani ambapo viongozi wao wa kamati ya mashindano walitinga na kushuhudia maandalizi hayo.
Wakiongozwa na mwenyekiti wao Isaac Chanji aliyeambatana na wajumbe wake Musa Katabaro,Said Ntimizi na Ndama mara baada ta mazoezi hayo walikutana na kikosi hicho katioka hoteli yao na kuwaachia kiasi cha sh milioni 6 ikiwa ni fedha za vocha.
Viungo Nizar Khalfan mwenye mpira mbele ya Haruna Niyonzima mazoezini leo
Said Juma 'Kizota' akimtoka Hassan Dilunga
Matajiri wa Yanga SC, Mussa Katabaro kulia na Rashid Ntimizi kushoto

Akizungumzia maandalizi yao Kocha Mkuu wa timu hiyo Hans Pluijm amefarijika na morali ya wachezaji wae ambapo amesema wanataka kupata ushindi katika mechi zao.
"Unaona jinsi wachezaji wanavyojituma hii ni ishara kwamba tunataka kupata mafanikio katika mechi zetu kuanzia hii ya Jumapili,"amesema Pluijm.

0 maoni:

Post a Comment