NYOTA
ya mshambuliaji Javier Hernandez ‘Chicharito’ imeendelea kung’ara baada
ya kuifungia mabao mawili Real Madrid ikiibuka na ushindi wa 4-2 dhidi
ya wenyeji Celta Vigo Uwanja wa Balaidos katika mchezo wa La Liga usiku
wa kuamkia leo.
Real
sasa inapunguza pengo la idadi ya pointi inazozidiwa na vinara wa La
Liga, Barcelona hadi kubaki pointi mbili (81-79), timu zote zikiwa
zimecheza mechi 33.
Wenyeji
ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya tisa kupitia kwa Nolito,
kabla ya Real kusawazisha kupitia kwa Toni Kroos dakika ya 16 na
Chicharito akafunga la pili dakika ya 24.
Hata
hivyo, wenyeji wakasawazisha tena dakika nne baadaye kupiria kwa Mina,
kabla ya James Rodriguez dakika ya 43 na Chicharito dakika ya 69
kuifungia Real bao la tatu na la nne.
Chicharito
ndiye aliyeifungia Real bao pekee la ushindi katika Robo Fainali ya
Ligi ya Mabingwa dhidi ya Atletico Madrid, lakini Nahodha wa zamani wa
Arsenal, Thierry Henry akamkandia ‘kinoma’.
Alisema
alishangilia kama ametwaa Kombe la Dunia- na alishangilia bila ya mtu
aliyemoa pasi, Ronaldo ambaye ndiye alifanya kazi kubwa. Na Henry ambaye
sasa ni mchambuzi wa Sky Sports, akasema Chicharito anayecheza kwa
mkopo kutoka Manchester United, hakucheza vizuri na hana uhakika kama
atapewa nafasi zaidi kikosini Real.
Javier Hernandez akishangiia baada ya kuifunjgia Real Madrid mabao mawili jana
0 maoni:
Post a Comment