VIUNGO
wa zamani wa kimataifa wa England, Steven Gerrard na Frank Lampard
usiku huu wamepewa tuzo kutokana na mchango wao mkubwa katika Ligi Kuu
ya England.
Wawili hao
wanaohamia Marekani mwishoni mwa msimu baada ya kucheza England kwa
muda mrefu, wamepewa tuzo hizo na Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA)
usiku huu.
Wote
Gerrard na Lampard wanapewa heshima ya wachezaji wa 'kizazi cha dhahabu'
England na kwa pamoja wameichezea timu ya taifa mechi 220 baina yao.
Steven Gerrard na Frank Lampard (kulia) wamepewa tuzo na PFA usiku wa jana.
0 maoni:
Post a Comment