May 2, 2015

HIKI NDIO KITUO KITAKACHO RUSHA LIVE MECHI YA YANGA LEO

AZAM TV, Televisheni namba moja Tanzania ya michezo na burudani- leo inatarajiwa kuonyesha moja kwa moja mchezo kati ya Yanga SC dhidi ya wenyeji Etoile du Sahel nchini Tunisia.
Mchezo huo utaanza Saa 1:00 usiku kwa Saa za Kaskazini mwa Afrika na Saa 3:00 usiku kwa Saa za Afrika Mashariki Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse na Azam TV wataanza Saa 2:00 kutoa maelezo ya utangulizi kupitia chaneli ya Azam Two. 
Etoile du Sahel wamethibitisha kufikia makubaliano na Azam TV kurusha mchezo huo ‘Live’ leo.  
Aidha, kamera za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) zimezuiwa Uwanja wa Ndege wa Tunis. 
Watangazaji wa TBC wakiongozwa na Enock Bwigane walizuiwa kutoka na kamera na wakalazimika kuziacha kwenda kuripoti mechi hiyo.
Hakuna tatizo kwa Waandishi wa Habari kuingia Tunisia, bali kamera za video ndizo zimezuiwa na wakati wafanyakazi wa TBC wanarejea nyumbani watakabidhiwa vifaa vyao.

0 maoni:

Post a Comment