May 2, 2015

KAVUMBAGU APONDEA TUZO ZA KILA MWEZI VPL, ADAI ZINAENDESHWA KWA KUJUANA

kavumbagu 222Na. Richard Bakana, Dar Es Salaam
Mshambuliaji wa klabu ya Azam FC, Didier Kavumbagu, amefunguka ya moyoni juu ya muenendo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ambayo inaelekea ukingoni na kusema kuwa inaendeshwa kwa kujuana zaidi.

Akizungumza na Shaffihdauda.com Mshambuliaji huyo ambaye alijiunga na Azam FC mwaka jana akitokea Yanga SC, amesema kuwa kutokana na mchango ambao anauonyesha katika klabu yake hasa pale mwanzoni mwa ligi, alikuwa anastahili kupewa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Septemba 2014, lakini anadai kuwa kujuana ndio kulipelekea akanyimwa na kupewa mchezaji wa Mbeya City Antony Matogolo licha ya timu yake kufanya vibaya kwa wakati huo.
“Unaweza kusema ligi inaenda kwa kujuana, ilitakiwa nipewe tuzo ya mchezaji bora mwezi Januari lakini akapewa wa Mbeya City, Ukiangalia Muda huo nilikuwa ninafunga katika kila mechi huku timu yangu ikifanya vizuri lakini nikanyimwa akapewa yeye wakati timu yake ilikuwa inafanya vibaya” Amesema Didier Kavumbagu.

Wadhamini wakuu wa Ligi hiyo ambao ni kampuni ya Simu za mkononi Vodacom, Mwaka jana walikuja na wazo la kutoa tuzo kwa mchezaji bora wa mwezi kufatia kazi nzuri na mchango wao katika timu, zoezi ambalo lilipokelewa vizuri na kusimamiwa vyema na TFF wakishirikiana na Bodi ya ligi ambao waliteua watu maalumu (Makocha) ili kuhakikisha mshindi anapatikana kwa haki na kwakuzingatia vigezo husika, Kigezo kimojawapo kikiwa ni Mchezaji awe ameisaidia timu yake kufanya vizuri ndani ya mwezi husika.
Hadi Matogolo anakabidhiwa tuzo hiyo ikiwa ni kabla ya Mbeya city kumpeleka Panone FC kwa mkopo, Wagonga Nyundo hao wa jiji la Mbeya tayari walikuwa wamepoteza michezo minne mfululizo huku Azam FC ikichanja mbuga katika kutetea Ubingwa ilioupata msimu uliopita bila kufungwa pamoja na Mtibwa Sugar, Tukio ambalo lilifanya wachambuzi wengi wa soka Tanzania kushangaa na kujiuliza ni vigezo gani ambavyo TFF na Bodi ya Ligi walitumia hadi kumpatia mchezaji huyo tuzo na kuwaacha watu kama Kavumbagu na Ame Ally ambao kwa muda ule ndio waliokuwa wanafanya vizuri sana.

Michezo ambayo Mbeya City ilipoteza Antony Matogolo akicheza ni dhidi ya Ruvu Stars zilitoka sare tasa Septemba 20, Septemba 27 Mbeya City 1-0 Coastal Unon. Oktoba 4, Ruvu Shooting 0-0 Mbeya City. Oktoba 18, Mbeya City 0-1 Azam FC. Oktoba 26, Mbeya City 0-2 Mtibwa Sugar. pamoja na ule mchezo wa mwanzoni mwezi Novemba ambapo City walikutana na JKT Mgambo wakapoteza kwa bao 2-1 Mkwakwani Tanga.

Kavumbagu ameiambia Shaffihdauda.com kuwa kama kweli haki na sheria zote zingefatwa basi yeye ndio angeibuka kinara wa tuzo hiyo ambayo inathamani ya Pesa za Kitanzania Milioni Moja.

Mbali na Antony Matogolo kunyakua tuzo hiyo baadhi ya wachezaji wengine ambao wamewahi kuchukua tuzo hiyo ni pamoja na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ wa Azam FC (Oktoba), Rashid Mandawa wa Kagera Sugar (Novemba), Mahundi (Desemba), Said Bahanunzi wa Polisi Moro (Januari) na Godfrey Wambura wa Coastal Union (Februari).

0 maoni:

Post a Comment