Uongozi wa Stand United umelalama kuwa Simba imekuwa hailipi kasi cha mshahara kwa mshambuliaji Haruna Chanongo.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Stand United, Mhibu Kanu amesema makubaliano yao na Simba ni kila upande kulipa nusu mshahara lakini Simba wamekuwa hawafanyi hicho.
"Sisi tumekuwa tukitekeleza, lakini wenzetu mambo yamekuwa tofauti. Hawamlipi na hili tunaona wanapunguza utendaji wake maana wanamvunja nguvu.
"Tuko katika mazungumzo tujue inakuwaje lakini vizuri wangetekeleza mkataba," alisema Kanu.
Kwa upande wa Simba, Katibu Mkuu, Stephen Ally alisema wamekuwa wakimlipa Chanongo kupitia akaunti yake kama kawaida.
"Ni kweli tumekubaliana hivyo na Stand, kila upande umekuwa ukilipa nusu na sisi tunatimiza hilo kupitia akaunti yake.
"Huenda hajaenda kuangalia, namshauri angeenda kuangalia kabla ya kulalamika," alisema.
0 maoni:
Post a Comment