BAADA ya kufuta ukame wa kufunga
magoli katika mechi za ligi kuu, Mshambuliaji wa Simba, Danny Sserunkuma
amesema limekuwa jambo jema kwake kufunga magoli matatu mpaka sasa.
Danny amesema kazi ya mshambuliaji ni kufunga magoli na inapokuwa kinyume lazima presha iwe kubwa.
“Siku zote ni vizuri kwa
mshambuliaji unapoanza kufunga magoli na kuisaidia timu kupata ushindi,
hata nilipokuwa sifungi nilikuwa na furaha kwasababu timu ilishinda
kombe, lakini kwasasa nina furaha zaidi baada ya kuanza kufunga, kwa
mshambuliaji hili ni jambo nzuri.”Amesema Danny na kuongeza: “Siku zote
kuna presha, lakini kocha anatuambia tufurahie mchezo, tusiwazie
presha, siku zote presha ipo katika soka”.
Wakati huo huo, Emmanuel Okwi amesema anamfahamu vizuri Danny na amecheza naye timu ya taifa na hana wasiwasi na uwezo wake.
“Namjua Danny (Sserunkuma), ni
mfungaji mzuri, Kenya alifunga sana, kilichomsumbua hapa Tanzania ni
kukosa uzoefu na wachezaji wenzake, ona sasa amepata uzoefu na ameanza
kufunga”.
Simba ina wachezaji watano wa
Kigeni wote kutoka Uganda ambao ni Juko Mursheed, Joseph Owino, Danny
Sserunkuma, Emmanuel Okwi na Danny Sserunkuma.
0 maoni:
Post a Comment