Na. Richard Bakana, Dar es salaam
Timu ya Mwadui FC kutoka Mkoani
Shinyanga leo imefanikiwa kujihakikishia kiganjani tiketi ya kutinga
kunako ligi kuu ya Soka Tanzania bara Msimu wa 2015/2016 baada ya
kuichapa Polisi Tabora kwa jumla ya mabao 2-0.
Kupanda kwa Kikosi hicho kinacho
nolewa na Kocha wa Zamani wa Simba SC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio Albeto’
inafanya Mkoa wa Shinyanga kufikisha idadi ya Timu mbili zinazocheza
ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ikiungana na Stand United ‘Watoto wa
Mjini’.
Mchezo huo ulipata fursa ya
kutazamwa na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa TFF akiwemo
Mkurugenzi mkuu wa Mashindano ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania
Bwana Boniface Wambura.
Kufatia ushindi huo Mwadui
wanakuwa wamefikisha Pointi 43 mbele ya Toto Afrika ambao kabla ya
mchezo wa leo dhidi ya Geita Gold SC ambao umevunjika kufatia vurugu na
Mwamuzi kupokea kipigo, walikuwa na pointi 39 mbele ya JKT Oljoro na
Polisi Tabora waliokuwa na alama 38.
Mwaka jana Julio alitaka
kuipandisha timu hiyo ligi kuu lakini kufatia mambo kadha wa kadda ndani
ya TFF ikiwemo kuchelewa kutoa uamuzi wa nini kifanye baada ya mchezo
kati yao na Stand United kuvunjika hari iliyopelekea Kushindwa kutinga
VPL na Stand United kuchukua nafasi hiyo.
Hadi sasa Stand United ipo nafasi
ya pili kutoka mkiani yaani ya 13 ikiwa na pointi 11 mbele ya Tanzania
Prisons inayokamatilia mkia ikiwa na pointi 10 katika ligi kuu ya
Tanzania bara
0 maoni:
Post a Comment