Uongozi wa muziki nchini marekani unao muongoza msanii wa
R&B Chris Brown umetoa taarifa kwa uongozi wa muziki Tanzania unao
muongoza msanii kutoka Tanzania ALI KIBA msanii ambae yupo chini ya
uongozi wa Kampuni za SAMSUNG. Kwa taarifa zilizopo katika mtandao wa
VIP Beats nchini marekani zinaeleza kua tarehe 24 mwezi wa 11 mwaka 2014
uongozi wa msanii Chris Brown ulipokea maombi ya muungano wa wasanii
wawili kufanya wimbo wa pamoja kati ya msanii Ali kiba na Chris Brown
maombi hayo yaliambatanishwa na Softcopy zilizobeba nyimbo tatu za
msanii Ali kiba ikiwemo SINGLE BOY, MWANA pamoja na wimbo aliofanya
katika project ya ONE 8. Uongozi wa Chris Brown umethibitisha kupokea
taarifa za maombi hayo na umeonesha kupenda sauti ya msanii Ali kiba na
kutoa tamko kua wapo tayari kusimamia kazi ya pamoja itakayofanywa na
wasanii hawa. Upande wa msanii Chris Brown amesema hana tatizo yupo
tayari kushirikiana na msanii Ali kiba kwani alipata nafasi ya kutazama
project ya One 8 na ameona kiwango cha msanii Ali kiba kinaridhisha
japokua anahitaji marekebisho madogo sana.
Tunampongeza
msanii Ali kiba kwa juhudi zake tunamtakia kila lakheri katika kazi hii,
kuipata habari hii kamili tembelea mtandao wa VIP Beats, Channel 0 au
unaweza kuipata katika American Spring news.
0 maoni:
Post a Comment