Feb 10, 2015

NGASSA YANGA WAMEKIUKA MAKUBALIANO

MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Mrisho Ngassa amesimulia machungu ya kimkataba anayokutana nayo ndani ya Yanga, lakini akawaambia viongozi wa klabu hiyo kumlipia deni alilolazimishwa kukopa ili aisaidie klabu hiyo.
 
Akizungumza mchana huu katika makao makuu ya klabu ya Yanga Ngassa amesema awali wakati anajiunga na Yanga akitokea Azam alipata ofa kubwa kutoka kwa El Merreikh ya Sudan, lakini hakuweza kusaini nao mkataba kutokana na tayari alishasaini mkataba na Yanga na kuamua kuwatosa Waarabu hao.
Mrisho Ngassa kushoto akizungumza na Waandishi wa Habari leo

Ngassa amesema mara baada ya kujiunga na Yanga akitokea Simba alikokuwa kwa mkopo kuliibuka deni la Sh Milioni 45 alilotakiwa kuwalipa Simba na uongozi wa Yanga ulimtafutia mkopo ambao alitakiwa kusaini ili umsaidie kulipa deni jambo ambalo hakukubaliana nao.
"Sikuwa tayari kusaini mkopo ule, niligoma kabisa lakini wakanilazimisha wakiniahidi kwamba klabu nayo itanisaidia kulipa lakini baadaye mambo hayakuwa hivyo, nilikatwa peke yangu,"alisimulia Ngassa.
"Kuna kipindi ambacho wakati nakatwa hizo fedha kumbe benki zilikuwa hazifiki, sikuwa najua zilikuwa zinaenda wapi lakini katika mshahara wangu zilikuwa zinakatwa."
 
Mshambuliaji huyo mwenye mabao mawili katika Ligi Kuu Bara huku pia akishikilia rekodi ya mfungaji Bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita, ameitaka Yanga kumlipia deni lake na endapo watafanya hivyo anaweza kuifungua mabao mengi zaidi kwa kuwa uwezo wa kufanya hivyo anao.
Awali akizungumzia sakata hilo la Ngassa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Yanga ,Jerry Murro ametamka kwamba klabu yake haina mgogoro wowote a mchezaji huyo na tayari wameanza mazungumzo ya kuongeza mkataba

0 maoni:

Post a Comment