Feb 9, 2015

WENGER HAJUI WILSHERE ATARUDI LINI

 
Wilshere hajacheza tangu Novemba alipoumia kifundo cha mguu katika mechi ya Ligi Kuu ya England ambapo Arsenal ilifungwa mabao 2-1 na Manchester United.
Alikua arejee mazoezini lakini kabla ya mechi ya Jumanne dhidi ya Leicester City, Wenger alisema: "Lazima tumchunguze kila siku. Sijui lini ataweza kurejea uwanjani."

Kuhusu mchezaji mwingine Alexis Sanchez ambaye tayari amefunga mabao 18 msimu huu, Wenger alisema, “ Atajiunga na kikosi “ kitakachocheza na Leicester na kwamba hakukuwepo majeruhi wowote katika mchezo wa Jumamosi ambapo Arsenal walishindwa na watani wao wa jadi Tottenham. Kwa kupoteza mechi hiyo Arsenal sasa inashiikilia nafasi ya sita katika Ligi Kuu.


Mbali na Wilshere na Sanchez Arsenal pia inamkosa Alex Oxlade-Chamberlain ambaye aliumia wakati Arsenal ilipopambana na Manchester City mnamo mwezi uliopita.

0 maoni:

Post a Comment