Feb 9, 2015

WAAMUZI MECHI YA AZAM , YANGA HAWA HAPA

MAREFA kutoka nchi jirani za Burundi na Somalia, ndio watachezesha mechi za kwanza za Raundi ya Awali ya michuano ya Afrika za timu za Tanzania mwishoni mwa wiki.
Yanga SC itamenyana na BDF XI Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati Azam FC watakuwa wenyeji wa El Merreikh ya Sudan Jumapili Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji.
Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Azam na El Merreikh refa atakuwa Hassan Mohamed Hagi, wasaidizi wake namba moja Bashir Sh Abdi Sule na namba mbili Salah Omar Abubakar wakati mezani atakuwa Kidane Melles Terfe, wote wa Somalia.
Kikosi cha Azam FC kilichotolewa mapema Kombe la Shirikisho mwaka jana na Ferroviario mwaka jana

Kamisaa wa mchezo huo atakuwa M.CHaileyesus Bazezew Beleti kutoka Ethiopia.
Mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Yanga SC na BDF XI, refa atakuwa Thierry Nkurunziza, wasaidizi wake Ramadhani Nijimbere namba moja, Herve Kakunze namba mbili na mezani George Gatogato, wote wa Burundi wakati Kamisaa atakuwa Joseph Nkole wa Zambia.

0 maoni:

Post a Comment