TIMU
ya Taifa ya Ivory Coast imetwaa Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya
kuifunga Ghana kwa penalti 9-8 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 120
Uwanja wa Bata, Equatorial Guinea.
Historia
imejirudia, baada ya Tembo kuwaunga ten Black Stars kwa penalti katika
fainali kama ilivyokuwa 1992 walipotwaa taji lao la kwanza.
Shujaa
wa Ivory Coast usiku huu alikuwa ni kipa Boubacar Barry aliyefunga
penalti ya mwisho, akitoka kuokoa ya kipa mwenzake, Razak Braimah na
kumaliza kiu ya miaka 23 ya taifa lake kusubiri taji hilo.
Penalti
za Ivory Coast zilifungwa na Aurier, Doumbia, Yaya Toure, Soomon Kalou,
Kolo Toure, Kanon, Bailly Serey Die na Barry, wakati Wlifried Bony na
Tallo walikosa mbili za kwanza.
Penalti
za Ghana zilifungwa na Mubarak Wakaso, Joedan Ayew, Andre Ayew, Mensah,
Agyemang-Badu, Afful, Baba na Boye wakati Acquah, Achwampong na Brimah
walikosa.
Rais wa
Equatorial Guinea, Teodoro Obiang, Rais wa FIFA, Sepp Blatter na Rais wa
CAF, Issa Hayatou walikuwepo uwanani na awali walikagua vikosimkabla ya
kukabidhi Medali na taji kwa washindi baada ya mechi
Kikosi
cha Ivory Coast kilikuwa; Barry, Bailly, Aurier, Kanon, Toure,
Tiene/Kalou dk114, Die, Toure, Gradel/Doumbia, dk66, Bony na
Gervinho/Tallo, sk120.
Ghana;
Razak, Boye, Rahman, Mensah, Afful, Mubarak, Acquah, Ayew,
Atsu/Acheampong dk115, Gyan/Agyemang-Badu dk120 na Appiah/Ayew dk98.
Wachezaji
wa Ivory Coast na viongozi wao wakifurahia na Kombe la Mataifa ya
Afrika baada ya ushindi wa penalti 9-8 dhidi ya Ghana usiku huu
Mshambuliaji wa Manchester City, Wilfried Bony akiwa amembeba kipa Boubacar Barry baada ya kufunga penalti ya mwisho mjini Bata
0 maoni:
Post a Comment