Mashabiki wa soka Misri huenda
safari hii wakasahau kwa muda ligi kuu ya nchini kwao baada ya Serikali
kutangaza kuisimamisha ligi hiyo kwa muda usiojulikana baada ya kuzuka
vurugu zilizotokea jana na kusababisha watu zaidi ya 20 kufariki.
Wengi wa waliofariki ni mashabiki wa timu ya Zamalek
ambao walifariki kutokana na msongamano mkubwa wa watu waliokuwa
wakijaru kuingia kwa nguvu uwanjani ambapo Polisi waliwafyatua mabomu ya
machozi wakati timu hiyo ilipokuwa ikipambana na timu ya ENPPI.Taarifa ya Wizara ya mambo ya ndani ya Misri inasema kuwa Mashabiki wa Zamalekwalikuwa wanataka kuingia uwanjani kwa nguvu bila tiketi, Polisi walijikuta wakitumia nguvu ya ziada kuwazuia ili wasifanye uharibifu uwanjani.
Tukio hili limetokea ikiwa ni miaka mitatu tangu itokee ishu kama hiyo ambapo wapenzi wa soka zaidi ya 70 walifariki wakati vurugu zilizotokea katika uwanja wa ndege wa Port Said.
0 maoni:
Post a Comment