NAHODHA wa Ivory Coast, Yaya Toure
amesema kwamba klabu yake, Manchester City inatakiwa kushinda mechi
zote zilizobaki ikiwa inataka kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya England.
Akizungumza
baada ya kuwaongoza Tembo kushinda taji la Kombe la Mataifa ya Afrika,
Toure ambaye alikandiwa kwa kucheza chini ya kiwango kwenye baadhi ya
mechi za AFCON alisema yuko tayari kurudi kazini Man City.
Lakini klabu yake ikiwa inazidiwa pointi saba na vinara Chelsea, nyota huyo wa Ivory Coast amesema hiyo si kazi rahisi.
Yaya
Toure akipokea Kombe la Afrika jana mjini Bata, Equatorial Guinea baada
ya kuiongoza Ivory Coast kushinda kwa penalti 9-8, kufuatia sare ya 0-0
ndani ya dakika 120
"Kwa kujiamini kwangu, najua soka si kuhusu mchezo mmoja, au miwili hususan katika Ligi Kuu ya England,"amesema.
"Tuna mechi 38 na ikiwa tunataka kushinda (kutetea ubingwa) tunatakiwa kushinda mechi zote. "Nafahamu ni vigumu, lakini nafahamu natakiwa kurejea na kufanya kazi yangu tena,".
Toure
alifunga mkwaju wake wa penalti wakati matuta jana Ivory Coast
ikiibwaga Ghana 9-8 na kutwaa Kombe- na sasa anarejea England kuisaiedia
Man Citu viya ya kutetes taji baada ya kukosekana tangu mwezi uliopita.
Na Manchester City haijashinda mechi hata moija tangu Mwanasoka huyo Bora wa Afrika aende kwenye AFCON.
0 maoni:
Post a Comment