Feb 10, 2015

BEKI KISIKI YANGA KUWAKOSA WA BOTSWANA

YANGA SC itamkosa beki wake mahiri chipukizi, Edward Charles Manyama katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya BDF XI ya Botswana mwishoni mwa wiki.
Edward alitoka nje dakika ya 39 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bada jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya kuumia enka na nafasi yake ikichukuliwa na Juma Abdul.
Na leo Daktari wa Yanga SC, Juma Sufiani amesema mlinzi huyo wa pembeni kushoto atakuwa nje kwa siku 10 akiuguza maumivu yake, maana yake Jumamosi atakosekana.
Edward Charles jana baada ya kuumia

Lakini hapana shaka kuumia hadi kukosekana kwa beki huyo aliyesajiliwa msimu huu kutoka JKT Ruvu si pigo sana, kwa sababu yupo beki chaguo la kwanza katika nafasi hiyo, Oscar Fanuel Joshua.
Kuna uwezekano Charles akaukosa hata mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho, lakini hakuna shaka mapema Machi atakuwa fiti kabisa kuanza tena kufanya kazi Jangwani.

0 maoni:

Post a Comment