KLABU ya Manchester City inaendelea kumfuatilia kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone kwa ajili ya kumchukua.
Mabingwa
hao wa Ligi Kuu ya England, wameachwa pointi saba na vinara Chelsea
baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Hull City.
Timu
hiyo ya Manuel Pellegrini sasa ipo kwenye hatari ya kumaliza msimu bila
taji baada ya kutolewa kwenye mashindano yote ya nyumbani katika hatua
za mwanzoni. Mbali na mbio za ubingwa wa Ligi Kuu, zaidi Man City
itajaribu bahati yake kwenye hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Diego Simeone yuko kwenye rada za Manchester City
SUPER SIMEONE
7- Baada ya miaka tisa ya ukocha, Simeone tayari ameshinda mataji saba — yakiwemo La Liga, the Copa del Rey na Europa League.
64.3 ndiyo wastani wa asilimia za ushindi wake kwa misimu yake mitatu na nusu
4- Mara kadhaa, Simeone amewafunga wapinzani wake kama Real, na pia wametoa sare mbili
Februari
24, mwaka huu, Manchester City itamenyana na Barcelona kwa mara ya pili
mfululizo na kipigo kingine kwa Pellegrini kitaibua maswali juu ya
mustakabali wa Mchile huyo.
Simeone
aliiongoza Atletico kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Hispania,maarufu La Liga
pamoja na kufika fainali ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya, ambako walifungwa
na mahasimu wao, Real.
Lakini
Simeone akalipa kisasi cha kufungwa kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa,
kwa kuitandika 4-0 timu ya Carlo Ancelotti Jumamosi.
Muargentina
huyo mwenye umri wa miaka 44 ndiye anaonekana mtu aliye tayari zaidi
kumrithi Pellegrini. Wote Ancelotti na koca Bayern Munich, Pep Guardiola
hawategemewi kuondoka katika klabu zao, wakati Jurgen Klopp amekuwa na
msimu mbaya
0 maoni:
Post a Comment