Mashabiki wa Yanga wapatao 160 wamekodi boti kuja jijini Dar kuongeza nguvu.
Yanga inashuka kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar kuivaa BDF XI ya Botswana katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho.
Wanachama na mashabiki hao wanasafiri kwenda jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuisaidia timu yao kwa kushangilia kwa nguvu.
Mmoja wa wanachama wa Yanga kutoka Zanzibar, Mohammed Hamis amesema wamekuwa wakichangishana kwa zaidi ya wiki moja sasa.
"Yanga ni timu ambayo inawakilisha taifa, tumeona tuwe na wawakilishi Dar es Salaam siku ya mechi.
"Tayari tumeanza kuandikisha majina kwa wale wanaotaka kwenda na michango imekuwa ikitolewa.
"Tunaamini idadi inaweza kuzidi hata hao watu mia sitini maana mwamko ni mkubwa sana," alisema.
0 maoni:
Post a Comment