MECHI
kati ya Arsenal dhidi ya Manchester United wakati wote imekuwa moja ya
michezo ya kusisimua katika historia ya Ligi Kuu ya England – lakini
The Gunners wameshinda mechi moja tu kati ya 11 zilizopita baina ya
klabu hizo.
Louis
van Gaal atasafiri na kikosi chake chenye majeruhi kibao hadi Uwanja wa
Emirates Jumamosi mchana akitambua kwamba timu yake imekuwa na historia
nzuri siku za karibuni dhidi ya wapinzani wake hao.
Licha
ya kuboronga msimu uliopita, lakini bado United ilijimudu kuichapa
Arsenal 1-0 Uwanja wa Old Trafford na kutoka nayo sare ya bila kufungana
katika mchezo mwingine Kaskazini mwa London.
Aaron Ramsey alifunga bao pekee mara ya mwisho Arsenal ilipoifunga Manchester United mwaka 2011
Arsenal iliifunga Manchester United 1-0 mwaka 2011 - ushindi wao pekee katika mechi 11 dhidi ya United
Danny
Welbeck - ambaye kwa sasa yupo Arsenal - alifunga bao la ushindi dakika
ya mwisho Manchester United ikishinda Uwanja wa Emirates mwaka 2012
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Robin van Persie alifunga bao la ushindi kwa United Uwanja wa Old Trafford msimu uliopita
Feb 12, 2014 | Arsenal | 0-0 | Man Utd |
Nov 10, 2013 | Man Utd | 1-0 | Arsenal |
Apr 28, 2013 | Arsenal | 1-1 | Man Utd |
Nov 3, 2012 | Man Utd | 2-1 | Arsenal |
Jan 22, 2012 | Arsenal | 1-2 | Man Utd |
Ago 28, 2011 | Man Utd | 8-2 | Arsenal |
May 1, 2011 | Arsenal | 1-0 | Man Utd |
Dec 13, 2010 | Man Utd | 1-0 | Arsenal |
Jan 31, 2010 | Arsenal | 1-3 | Man Utd |
Ago 29, 2009 | Man Utd | 2-1 | Arsenal |
May 16, 2009 | Man Utd | 0-0 | Arsenal |
Wakati
kocha Sir Alex Ferguson akiwa katika msimu wake wa mwisho Old Trafford,
mabao ya Robin van Persie na Patrice Evra yaliipa United ushindi wa 2-1
nyumbani wakati Van Persie pia alifunga tena dhidi ya Arsenal
aliporejea Emirates baadaye msimu huo kusawazisha baada ya Theo Walcott
kuanza kufunga na kufanya sare ya 1-1.
Ushindi
wa mwisho wa Arsenal katika Ligi Kuu ya England dhidi ya United ulikuwa
Mei mwaka 2011 wakati Aaron Ramsey alipofunga bao pekee katika ushindi
wa 1-0 nyumbani.
Kutoka
kwenye kikosi cha Arsenal wakati huo, wachezaji watano bado wapo
klabuni, akiwemo kipa Wojciech Szczesny, Laurent Koscielny, Walcott,
Ramsey na Jack Wilshere.
Lakini
ikiwa Wenger anatafuta ahueni anahitaji kutazama juu ya rekodi ya
ugenini ya United, bado hawajashinda mechi yoyote ugenini msimu huu na
hawajachukua pointi tatu katika mechi zao za ugenini tangu Aprili 5,
mwaka huu walipoifunga Newcastle 4-0.
Misimu
iliyopita, mechi kati ya Arsenal vs Manchester United ilikuwa ya kuamua
bingwa, lakini mwaka huu inaonekana kama ni mechi ya kuwania nafasi ya
nne na ya mwisho ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Lakini kikubwa zaidi, The Gunners wanatarajiwa kufuta uteja wao kwa United.
0 maoni:
Post a Comment