MANCHESTER United
imeendeleza ubabe dhidi ya Arenal, baada ya usiku huu kuichapa mabao 2-1
Uwanja wa Emirates katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
United walipata bao la kwanza dakika ya 56, baada ya beki Kieran Gibbs
kumfunga mwenyewe kipa wake, Wojciech Szczesny katika harakati za kuokoa
krosi ya Antonio Valencia, kabla ya Nahodha Wayne Rooney kufunga la
pili dakika ya 85 akimalizia pasi ya Angel di Maria. Olivier Giroud
aliifungia Arsenal la kufutia machozi dakika ya 90.
Beki wa United, Luke Shaw alitolewa nje dakika ya 16 baada ya kuumia
kifundo cha mguu, wakati kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere alinusurika
kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Marouane Fellaini.
Lakini kiungo huyo wa England alitolewa nje dakika ya 55 baada ya kuumia
pia. Kipa Szczesny pia alitolewa uwanjani baada ya kuumia.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny/Martinez dk59, Chambers,
Mertesacker, Monreal, Gibbs, Ramsey/Giroud dk77, Arteta,
Wilshere/Cazorla dk55, Oxlade-Chamberlain, Welbeck na Sanchez
Manchester United; De Gea, Smalling, McNair, Blackett, Valencia,
Carrick, Fellaini, Di Maria, Shaw/Young dk16/Fletcher dk89, Rooney na
Van Persie/James Wilson dk75.
Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney (kulia) akishangilia baada ya
Kieran Gibbs kujifunga
Woljciech Szczesny na Kieran Gibbs wa Arsenal wakipamiana kabla ya
kujifunga
PICHA ZAIDI NENDA:
http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2837001/Arsenal-vs-Manchester-United-Team-news-kick-time-probable-line-ups-odds-stats-Premier-League-clash.html#ixzz3JpEIaEU5
Make Money at : http://bit.ly/copy_win
Make Money at : http://bit.ly/copy_win
0 maoni:
Post a Comment