MSHAMBULIAJI
wa Bracelona, Lionel Messi ndiye mchezaji anayelipwa zaidi kwa sasa
duniani, akiwa anaingiza karibu Pauni Milioni 1 kwa wiki kutokana na
mshahara na mikataba ya udhamini.
Nyota
huyo wa kimataifa wa Argentina aliingiza pauni Milioni 47.8 mwaka 2014
za udhamini pamoja na mshahara wa klabu yake, Pauni Milioni 26.
Miongoni
mwa wadhamini wa Messi ni Adidas, FIFA 15 na Turkish Airlines na hiyo
inampandisha juu ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Ureno. Mreno huyo, Ronaldo, aliingiza Pauni Milioni 39.7, kwa mujibu wa taarifa zilizotoka sasa za Jarida la Wanasoka Tajiri.
Kwa
upande wa makocha, Mreno Jose Mourinho wa Chelsea ndiye anaongoza pato
lake la mwaka likiwa ni Pauni Milioni 13.2, akifuatiwa na Mtaliano wa
Real Madrid, Carlo Ancelotti Pauni Milioni 11.4, Mspanyola wa Bayern Munich, Pep Guardiola Pauni Milioni 11.2, Mfaransa wa Arsenal, Arsene Wenger Pauni Milioni 8.3 na Mholanzi wa Manchester United, Louis van Gaal Pauni Milioni 7.3.
Lionel Messi anaongoza kwa utajiri miongoni mwa wanasoka duniani
+14
Cristiano Ronaldo anashika nafasi ya pili kwa Pauni zake Milioni 39.7
WACHEZAJI WANAOLIPWA ZAIDI DUNIANI
1. Lionel Messi Pauni Milioni 47.8
2. Cristiano Ronaldo Pauni Milioni 39.7
3. Neymar Pauni Milioni 26.8
4. Thiago Silva Pauni Milioni 20.2
5. Robin van Persie Pauni Milioni 18.8
6. Gareth Bale Pauni Milioni 17.5
7. Wayne Rooney Pauni Milioni 16.5
8. Zlatan Ibrahimovic Pauni Milioni 15.8
9. Sergio Aguero Pauni Milioni 15.6
10. Robert Lewandowski Pauni Milioni 14.8 kwa mwaka
MAKOCHA WANAOLIPWA ZAIDI DUNIANI
1. Jose Mourinho Pauni Milioni 13.2 kwa mwaka
2. Carlo Ancelotti Pauni Milioni 11.4
3. Pep Guardiola Pauni Milioni 11.2
4. Arsene Wenger Pauni Milioni 8.3
5. Louis van Gaal Pauni Milioni 7.3
6. Fabio Capello Pauni Milioni 6.6
7. Andre Villas-Boas Pauni Milioni 6.2
8. Sven-Goran Eriksson Pauni Milioni 5.9
9. Jurgen Klopp Pauni Milioni 5.3
10. David Moyes na Laurent Blanc Pauni Milioni 5.1
0 maoni:
Post a Comment