SIMON Happygod Msuva amesema
anajisikia furaha kuchukua ubingwa huku goli lake alilofunga
kwa kichwa dhidi ya Ruvu Shooting likijadiliwa mno kwenye mitandao ya
kijamii na kufananishwa na alilofunga mshambuliaji wa Manchester United
na Uholanzi, Robin van Persie kwenye fainali za kombe la dunia mwaka
jana nchini Brazil.
“Watu wanasema nilifunga kama
Robin Van Persie, wanajadili sana kwenye mitandao, haya ni mafanikio
kwangu, juhudi ndio siri ya mafanikio” Amesema Msuva.
Winga huyo anayeongoza orodha ya
wafungaji akiwa amefumania nyavu mara 17 msimu huu akifuatiwa na Amissi
Tambwe mwenye magoli 14 ameongeza kuwa ubingwa waliopata anafurahi
kuchangia kwa kiasi kikubwa na ataendelea kufanya vizuri.
“Huu ni mwanzo tu, kila siku
najifunza na kupunguza makosa, tuna kocha mzuri, tunaamini tutafanya
vizuri zaidi siku zijazo tukianzia na mechi ijayo dhidi ya Etoile du
sahel”. Amesema Msuva.
0 maoni:
Post a Comment