WANASOKA
wawili mahasimu, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wanaweza kujikuta
katika kikosi kimoja kucheza mechi ya UEFA All-Star itakayohusisha
wachezaji bora zaidi Ulaya, kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania.
Wanaweza
kuchezea 'Team South', nyota wa Ulaya Kusini ambao watatoka katika Ligi
za La Liga ya Hispania, Serie A ya Italia na Ligue 1 ya Ufaransa dhidi
ya 'Team North', nyota wa Ulaya Kaskazini wanaotoka Ligi Kuu ya England,
Bundesliga ya Ujermani na Ligi Kuu ya Urusi.
Gazeti
la Mundo Deportivo limeripoti kwamba kampuni ya Masoko imeiomba UEFA
juu ya mchezo huo na kupendekeza ifanyike kila mwaka baada ya kuvutiwa
na na mechi ya NBA All-Star baina ya Western na Eastern Conferences
(Kanda ya Mashariki na Magharibi).
Messi na Ronaldo wanaweza kuungana katika kikosi kimoja kucheza mechi kati ya 'North dhidi ya South' All-Star
WANAOTARAJIWA KUWAMO VIKOSI VYA ALL-STAR YA UEFA
South: Buffon; Danilo, Sergio Ramos, Pique, Thiago Silva; Messi, Pogba, Koke, Neymar; Cristiano Ronaldo, Ibrahimovic
North: Neuer; Terry, Hummels, Alaba; Robben, Di Maria, Silva, Reus; Alexis, Aguero, Hazard
Wachezaji
wa kuchezea timu hizo watachaguliwa kwenye mitandao kutokana na kura za
mashabiki na klabu moja haitapewa fursa ya kutoa zaidi ya wachezaji
watatu.
Lakini pamoja
na ukweli huo, uhondo wa mecbi hiyo utaletwa na nyota wa Barcelona,
Messi na Neymar kuungana na mahasimu wao wa Real Madrid, Ronaldo na
Gareth Bale.
Nyota
wengine wa Kusini wanaopewa nafasi kubwa ya kuwamo kwenye kikosi cha
'Team South' ni pamoja na mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Zlatan
Ibrahimovic na kiungo wa Juventus, Paul Pogba.
Upande
wa 'Team Kaskazini' bila shaka nyota kama washambuliaji wa Manchester
City, Sergio Aguero, Man United, Wayne Rooney, winga wa Chelsea, Eden
Hazard, winga wa Manchester United, Angel di Maria na kipa wa Bayern
Munich, Manuel Neuer wanatarajiwa kuwamo.
0 maoni:
Post a Comment