Harry Kane amesisitiza kuwa ataendelea kuichezea Tottenham baada ya tetesi kuenea kwamba Manchester United wanavutiwa naye.
Mchezaji huyo bora kijana wa mwaka wa PFA amekumbana na
swali kuhusu hatima yake ya baadaye mara tu baada ya kuwasili Malaysia
kuelekea mechi ya kirafiki ya Spurs dhidi Malaysia XI.
Nyota huyo mwenye miaka 21 ameweka wazi kuwa ana nia ya
kuendelea kuichezea Spurs chini ya kocha Mauricio Pochettino ambaye
alimnoa vizuri msimu uliopita na kufunga magoli 21 sambamba na kucheza
mechi ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England.
0 maoni:
Post a Comment