May 22, 2015

IVO MAPUNDA ATIMKIA OMAN, MIPANGO YA MUSLEY HIYO


Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
MAKIPA wote wa Simba SC, wakiongozwa na ‘mkubwa wao’ Ivo Mapunda watakwenda mafunzoni nchini Oman.
Ivo pamoja na kipa wa pili, Hussein Sharrif ‘Casillas’ na makipa wa timu ya vijana wanaokomazwa kikosi cha kwanza, Peter Manyika na Dennis Richard wanatarajiwa kuondoka wakati wowote kwenda Oman.
BIN ZUBEIRY inafahamu kwamba mipango ya makipa hao kwenda mafunzoni, imefanywa na mmoja wa wafadhili wa timu hiyo, Musley Al Ruweh.
Ivo Mapunda anatarajiwa kuwaongoza makipa wenzake wote Simba kwenda Oman kwa mafunzo maalum

Musley ambaye pia amegharamia safari ya kwenda Oman kwa kocha wa makipa Meja na kocha Msaidizi, Suleiman Matola hakupatikana alipotafutwa kuzungumzia safari hiyo, lakini BIN ZUBEIRY inafahamu ni wakati wowote kuanzia sasa.
Makipa hao wanatarajiwa kwenda kunufaika na mafunzo ya kocha wa makipa aliyebobea, Haroon Amur Al Siyabi ambaye mara kadhaa huja nchini kuwanoa makipa wa Simba SC.
Matola yeye ambaye kwa sasa anaendelea na mafunzo ya ukocha Dar es Salaam, anatarajiwa kwenda kupatiwa programu maalum ya kujiendeleza zaidi kielimu nchini humo.
Musley kulia ndiye amefanikisha safari ya makipa wa Simba SC mafunzoni Oman

0 maoni:

Post a Comment