May 28, 2015

‘KAPTENI’ HANS POPPE AWASHUKIA MAWAKALA UCHWARA BONGO

Na Hemed Kivuyo, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI kamati ya usajili ya timu ya soka ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amewatolea uvivu wale wanaojiita `mawakala `wa wachezaji hapa nchini waliyoanza kujitokeza Nyakati hizi za Usajili wakipanga bei za Wachezaji bila kufuata utaratibu.
Amesema kuwa wakati huu ambapo baadhi ya wachezaji wanaongezewa mikataba na wengine kusajiliwa katika timu Mbalimbali wamejitokeza watu wanajitambulisha kuwa maajenti wa wachezaji ambao hupanga Bei za wachezaji huku wakiwa hawatambuliki na Shirikisho la Soka Nchini TFF pamoja na Klabu anayochezea Mchezaji.
Amedai kuwa alisikia taarifa kuwa wamemuongezea Mkataba `Kinyemela` Mchezaji Ramadhani Singano `Messi` huku yeye Mwenyewe akiwa hana taarifa jambo ambalo si sahihi na watahakikisha wanachukua hatua za kisheria kwa aliyezusha jambo hilo.
Amedai kuwa wao walimuongeza Mkataba Mchezaji wao ( Singano) na kumuongezea Mshahara lakini anasikitika kusikia walimuongezea mkataba Kinyemela jambo ambalo litaleta taswira mbaya kwa jamii.
``Sisi tulimuongezea Mkataba Mchezaji wetu Singano ikawa ni Maika mitatu na tulifuata taratibu zote,sasa tunashangaa anajitokeza mtu anajiita ajenti anasema mchezaji alimaliza mkataba wake na anasema tulighushi,hilo jambo ni baya sana hatutokubali kuzushiwa uongo wakati mchezaji tulimuongezea mkataba ili kuboresha mshahara wake ``,Alisema Hanspope kwa ukali.
Captain huyo mstaafu wa jeshi ( JWTZ) alitahadharisha kuwa kama TFF na Vilabu havitochukua hatua za haraka basi maajenti bandia wataendelea kujitokeza na kuharibu sura ya mchezo wa Soka Nchini.
Hans Poppe kulia amewajia juu mawakala uchwara nchini

USAJILI SIMBA SC;
KUHUSU usajili unaondelea Mwenyekiti huyo wa kamati ya usajili amesema kuwa kwasasa wanaendelea kujaza nafasi zinazoonekana kutakiwa kujazwa na wanaangalia namna ya kuwapandisha baadhi ya wachezaji .
Amekiri kuwa ni kweli wapo katika mazungumzo na Mchezaji Balimi Busungu ambaye jana aliitwa katika Timu ya Taifa ambaye wamempa ofa yao na wanasubiri majibu ya mchezaji huyo.
Ameongeza kuwa kwasasa hawana wasiwasi wala haraka ya kusajili mchezaji kwa gharama kubwa sana na kwamba wamempa ofa mchezaji huyo kutoka Mgambo ya Tanga na endapo hatokubaliana nao hawatoangaika kumuongezea fedha kwakuwa wachezaji wenye viwango vikubwa wapo wengi.

TAIFA STARS;
Akitoa mawazo yake juu ya maendeleo ya Timu ya Taifa (TAIFA STARS) Pope amesema kuwa haoni sababu ya kumlaumu kocha mkuu wa timu hiyo Mart Nooj kwakuwa zipo sababu Nyingi zinazofanya Taifa Stars ifanye vibaya.
Amesema kuwa Michuano ya COSAFA siyo kigezo chakupima uwezo wa Mwalimu wa Timu ya Taifa huku akitetea kuachwa kwa baadhi ya wachezaji .
Ameongeza kuwa kuachwa kwa baadhi ya wachezaji katika timu ya Taifa kunategemea na mambo mengi na mojawapo ni tabia za baadhi ya wachezaji kutokuwa na Nidhamu ndani na Nje ya Uwanja.
``Mimi kwa mtazamo wangu sioni sababu ya kumlaumu mwalimu wa Timu ya Taifa eti kwasababu ya Michuano ya COSAFA,zipo sababu nyingi zinazotufanya tukwame ukiangalia huku chini tunapopswa kuanza wa watoto tumepuuza,yani tumepuuza mambo mengi sana ambayo inatupasa turudi nyuma kinyume na hapo tutafukuza makocha wengi sana``. Alisema .

0 maoni:

Post a Comment