BONDIA Floyd Mayweather amemuita mpinzani wake Manny Pacquiao mwoga na amekataa pambano la marudiano.
Mayweather
alishinda kwa pointi katika 'Pambano la Karne' la utajiri wa Pauni
Milioni 300 mjini Las Vegas mwishoni mwa wiki iliyopita.
Pacquiao
baadaye akasema kwamba aliumia bega wiki mbili na siku kadhaa kabla ya
pambano akiwa mazoezini na tayari amesema amefanyiwa upasuajji Jumatano.
Manny Pacquiao baada ya mechi alisema aliumia bega wiki kadhaa kabla
Baada
ya pambano hilo, Mayweather alimtumia ujumbe wa maandishi mtangazaji wa
ESPN kwamba atajiandaa kwa pambano la marudiano na Pacquiao atakapopona
majeruhi yake.
Lakini
sasa amegeuza kibao na hataki tena kukutana ulingoni na Mfilipino huyo
badala yake anaelekeza nguvu zake kwenye pambano la 49 Septemba mwaka
huu na mpinzani mwingine.
"Nilimtumia ujumbe Stephen A Smith kumuambia nitapigana naye (Pacquiao)? Ndiyo, nimebadilisha mawazo," amesema.
"Kwa
wakati huu sasa, hapana, kwa sababu ni kibonde na mwoga. Kama umepigwa,
kubali kupigwa na sema, 'Mayweather, ulikuwa mpiganaji bora.'
Mayweather awali alikubali kurudiana Pacquiao, lakini amebadilisha mawazo
0 maoni:
Post a Comment