Uongozi wa Simba umesema utaanza rasmi kujenga uwanja wao wa mazoezi mwezi ujao.
Rais wa Simba, Evans Aveva amesema watautumia uwanja wao wanaoumiliki kuanza kujenga uwanja wa mazoezi.
“Tutaanza
kujenga uwanja kwa ajili ya mazoezi kwa ajili ya kupunguza gharama, kwa
siku tunalazimika kulipa hadi laki tatu na nusu kwa mazoezi ya mara
moja.
“Kulikuwa
kuna mambo ya kupata hati ya umiliki, wakati tunaingia kulikuwa na deni
kama la shilingi milioni kumi na mbili hivi,” alisema Aveva.
Uwanja huo ulio katika eneo la Bunju jijini Dar es Salaam, ulinunuliwa na uongozi chini ya Hassan Dalali aliyekuwa mwenyekiti wakati huo
0 maoni:
Post a Comment