Feb 20, 2016

ALICHOSEMA TAMBWE BAADA YA YANGA KUPATA USHINDI DHIDI YA SIMBA

Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe ambaye amefunga bao la pili katika mechi ya leo ambapo Yanga imeilaza Simba kwa mabao 2-0. Beki Abdi Banda alilambwa kadi ya njano ya pili katika dakika ya 25 na kuzaa nyekundu baada ya kumwangusha Donald Ngoma.

Tambwe alifunga bao katika dakika ya 72 baada ya beki Juuko Murshid kushindwa kumdhibiti baada ya krosi safi ya Geofrey Mwashiuya.
“Tulianza vizuri, mechi ilikuwa na
ushindani mkubwa. Lakini baada ya ile kadi nyekundu, ilitusaidia sisi kuingia kwa wingi katikati na kuwabana Simba.

Mechi ilikuwa nina ushindani sana, Simba walijitahidi kucheza vizuri licha ya kuwa pungufu. Lakini sisi tulikuwa bora zaidi leo,” alisema Tambwe raia wa Burundi.
Hilo ni bao la 15 msimu huu, huku akiwa amebakiza bao moja tu kumkamata Amissi Kiiza ambaye ana mabao 16.

0 maoni:

Post a Comment