Feb 2, 2016

CHANONGO UBWA MAMBO SAFI TP MAZEMBE

Na Haji Balou

KLABU ya TP Mazembe ya DRC
imeingia katika mazungumzo ya
kuwanunua wachezaji wawili wa
Stand United, beki Abuu Ubwa na
kiungo Haroun Chanongo baada ya
kufanya vizuri katika majaribio yao
mapema Januari.

Wawili hao walisafiri hadi
Lubumbashi, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC),
mapema Januari kwa majaribio ya
wiki moja na taarifa za awali
zikasema, wamefuzu.
Meneja wa wachezaji hao, Jamal
Kisongo amesema tayari Mazembe
imetuma barua rasmi ya majibu ya
majaribio ya vijana hao na kwamba
sasa wanaingia katika mazungumzo
na klabu yake.
“Jana nimepokea taarifa rasmi kutoka Mazembe kwamba (Chanongo na Ubwa) wamefuzu. Tunatarajia watasaini Mkataba wakati wowote baada ya kukamilika kwa mazungumzo na klabu yao,”amesema Kisongo akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo.

Kisongo ambaye pia ni Meneja wa
mshambuliaji wa KRC Genk ya
Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta
amesema kwamba mazungumzo
rasmi yatafanyika baada ya Rais wa
Mazembe, Moise Katumbi kurejea
Lubumbashi kutoka Ulaya.

0 maoni:

Post a Comment