Mar 3, 2016

BAADA YA ISIHAKA KUFUNGIWA SIMBA HAYA NDIO ALIYOSEMA HAMISI KIIZA

Na Haji balou


Mshambuliaji wa Simba, Hamisi Kiiza naye yuko katika wakati mgumu baada ya kuandika mambo mtandaoni akionyesha kuupinga uongozi wa Simnba kumsimamisha nahodha wake, Hassan Isihaka.

Simba ilitangaza kumfungia Isihaka kwa muda usiojulikana kutokana na kitendo chake cha kumtolea mwalimu wake, Jackson Mayanja maneno yasiyo ya kiungwana.


Taarifa kutoka ndani ya Simba zimeeleza, Kiiza ameanza kujitetea akitupia lawama magazeti. Kwamba yaliandika na kumchafua Isihaka.

Lakini hali halisi inaonyesha haikuwa hivyo kwani yeye alianza kutupia mtandaoni hata kabla ya magazeti kuandika.

Presha imekuwa kubwa kwa Kiiza baada ya uongozi kumtaka aombe radhi. 

Lakini presha ikawa kubwa zaidi baada ya mhusika mwenyewe, Isihaka kuona amefanya kosa na kuamua kumuomba radhi kocha wake na uongozi.


Kiiza alitupia maneno kwenye mtandao wa Instagram akidai Isihaka anachafuliwa. Jambo lililoonyesha wazi alikuwa akiupinga uongozi. Lakini hakueleza kama alikuwa akiunga mkono nahodha huyo kinda amjibu kocha wake hovyohovyo.

0 maoni:

Post a Comment