Jun 4, 2016

IBRAHIMOVIC ATAJIUNGA NA TIMU HII ENGLAND

Na Haji balou
Sky Sport wameripoti kuwa Zlatan Ibrahimovic  atakamilisha
usajili wa kujiunga na Man United wakati
wowote kuanzia sasa ila ni kabla ya michuano
ya mataifa ya Ulaya kuanza, Sky Sport
wanaeleza kuwa kocha wa Man United Jose
Mourinho amepanga kusajili mshambuliaji
mmoja katika dirisha hili la usajili ila Zlatan
Ibrahimovic ndio chaguo lake.

Mtendaji mkuu wa Man United Ed Woodward na
wawakilishi wa Zlatan wanaripotiwa kuwa katika
mazungumzo ya mwisho ili kumsajili staa huyo
kwa mkataba wa mwaka mmoja, Zlatan kwa
sasa yupo na timu yake ya taifa ya Sweden
anajiandaa mchezo wao wa kwanza wa Euro
2016 dhidi ya Ireland utakaochezwa June 13.

0 maoni:

Post a Comment