Na Haji balou
Msanii mkongwe wa muziki, Abbas Hamisi
Kinzasa ‘20%’ amerudi katika label yake ya
zamani ‘Combination Sound’ inayosimamiwa na
mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini Man
Water.
Muimbaji huyo ambaye mwaka 2011 alitwaa
tuzo saba za Kilimanjaro Music Award (KTMA)
kwa mara moja, huku producer wake Man Water
akichukua tuzo mara mbili mfululizo za producer
bora (mwaka 2013 na 2014), tayari
amesharekodi ngoma kadhaa chini ya producer
huyo.
Kupitia instagram, Man Water ameandika:
Twenty Percent is back 2016, kaa mkao wa kula
ngoma zenye jumbe nzito na za kusisimua, kila
kitu kiko sawa sasa, new page.
20% kwa sasa anajipanga kuachia wimbo wake
mpya utaotoka Julai 18 mwaka huu huku
akijapanga kuandaa albamu yake iitwayo ‘Sauti
ya Gharama’.
0 maoni:
Post a Comment