Na Haji balou
Mchezaji wa timu ya Simba Peter manyika Jr amesema yeye ni mmoja kati ya wachezaji wenye nidhamu isipokuwa mashabiki wengi wanamsema kutokana Na jinsi wanavyo mwona.
Manyika alisema hayo alipokuwa akihojiwa Na Sauda mwilima kupitia kipindi cha Mcheza kwao kinachorushwa na channeli ya Star Tv.
Pia alipoulizwa kuhusu skendo za mapenzi zinazo mkabili Manyika alisema kuwa "Siku zote ukiwa maarufu watu watazungumzia sana mahusiano yako kutokana Na aina ya mpenzi ambaye unatoka nae".
"Kiukweli Mimi nipo Na mpenzi wangu huyu huyu ambae ninae kwa miaka miwili sasa Ila kwakuwa watu wanaongea waache waongee" alisema Manyika Jr.
Mashabiki walianza kumtuhumu Manyika Jr anashuka kiwango baada ya kugundua anatoka kimapenzi na binti wa kiarabu ambaye anamfanya Manyika kushindwa kufanya mazoezi Mara kwa Mara.
0 maoni:
Post a Comment