Na Haji Balou
AKlabu za Ligi Kuu Bara kwa ajili ya msimu
mpya ligi kuu bara 2016/2017, kwa kuboresha
baadhi ya maeneo yenye mapungufu na
kuyaongezea nguvu.
Atupele Green (ametoka Ndanda kwenda
JKT Ruvu)
Mfungaji bora wa kombe la shirikisho FA na
klabu ya Ndanda kwa msimu uliomalizika
amemwaga wino kuitumikia JKT Ruvu kwa
msimu mpya, kwa uwezo wake mkubwa wa
kufumania nyavu atakua msaada mkubwa
kwa JKT Ruvu.
Mohamed Mkopi (ametoka Prisons kwenda
Mbeya City)
Moja ya matatatizo msimu uliomalizika
Mbeya city ni ubutu wa safu ya ushambuliji,
Mkopi ni mzuri kwenye kufunga na
kutengeneza nafasi za kufunga kwa wenzake,
kwa usajili huu Mbeya City watafaidika nao.
Hassan Kessy (ametoka Simba kwenda
Yanga)
Amesaini kuitumikia Yanga kwa miaka miwili,
usajili huu ni bora kwa Yanga sababu upande
wa beki ya kulia Yanga imekua aina mpinzani
kwa muda mrefu Juma Abduli amekuwa
akitawala, ujio wa Kessy Yanga utaleta
upinzani sahihi kwenye nafasi hiyo.
Shiza Kichuya (ametoka Mtibwa kwenda
Simba)
Mmoja wa viungo bora msimu uliomalizika
akiwa Mtibwa, amejiunga na Simba kwa ajili
ya msimu mpya, uwezo wake mkubwa
uwanjani utakuwa faida kwa Simba hapa ni
kama Simba imepiga bao kwa usajili wa
Kichuya.
Muzamili Yassin (ametoka Mtibwa kwenda
Simba)
Hakuna shaka na uwezo wa Muzamili ni
mmoja wa viungo bora chipukizi kwa msimu
uliomalizika, huu ni moja ya usajili bora
kwenda Simba kutokana na uwezo mkubwa
wa Muzamili kutengeneza nafasi za kufunga
kwa wenzake na ndicho kitu Simba walikuwa
wamekosa kwa kipindi kirefu tangu kuondoka
kwa Boban.
Edo Christopher (ametoka Toto kwenda
Kagera)
Kagera wanazidi kujiimarisha kwa ajili ya
msimu mpya baada ya kuponea kushuka
daraja msimu uliomalizika, ujio wa Edo
kwenye eneo la ushambuliaji utaongeza
chachu kutokana na uwezo wake wa kufunga
na uzoefu kwenye ligi kuu bara.
Juma Mahadhi (ametoka Coastal kwenda
Yanga)
Ni usajili bora kufanywa na Yanga kwa msimu
ujao, uwezo wake mkubwa kwenye mechi
dhidi ya Mazembe kwenye kombe la
shirikisho umeleta faraja kubwa kwa wapenzi
wa Yanga pamoja na wanachama.
Aziz Gilla (ametoka Mgambo JKT kwenda
JKT Ruvu)
JKT Ruvu wanajiimarisha kwenye maeneo
mbali mbali kwa ajili ya msimu mpya, ujio wa
winga mpya Aziz Gilla utakuwa msaada
kwenye timu yao hasa nidhamu yake na
uhamasishaji wa wenzake.
Vicent Andrew (ametoka Mtibwa kwenda
Yanga)
Amesaini Yanga kwa mkataba wa miaka
miwili licha ya ugumu wa namba kwenye
eneo analo cheza kwa sababu imejaza watu
wenye uzoefu lakini ni moja ya usajili bora
sababu ana uwezo wa kucheza namba zaidi
ya tatu uwanjani.
Dany Mrwanda (ametoka Majimaji kwenda
Kagera)
Kikubwa ni uzoefu wake kwenye ligi utakuwa
msaada mkubwa kwa Kagera timu ambayo
inajiimarisha kwa msimu mpya.
0 maoni:
Post a Comment