MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Robin van Persie ataikosa mechi ya kirafiki ya kimataifa baina ya nchi yake, Uholanzi dhidi ya Mexico Jumatano ya leo baada ya kocha Guus Hiddink kuthibitisha hayuko fiti kiasi cha kutosha.
Van
Persie akiwa Nahodha wa Uholanzi, aliiongoza hadi nafasi ya tatu katika
Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu nchini Brazil, lakini kikosi cha
Hiddink kimekuwa na wakati mgumu tangu baada ya michuano hiyo,
kikishinda mchezo mmoja tu katika mechi zao tatu za awali za kufuzu kwa
Euro.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 31, ambaye alicheza dakika zote 90 klabu yake
Man United ikimenyana na Crystal Palace mwishoni mwa wiki iliyopita,
anaweza akarejea kwa wakati kuivaa Latvia Jumapili.
Robin van Persie akiondoka kwenye mazoezi ya Uholanzi na kocha wa mazoezi ya viungo, Rene Wormhoudt jana
0 maoni:
Post a Comment