SIKU
chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kufanyiwa pasuaji wa tezi dume
(prostrate), mastaa mbalimbali wameguswa na kuunganisha nguvu ya pamoja
kumfanyia maombi mazito kiongozi huyo wa nchi ili aweze kupona
haraka.Rais Kikwete alifanyiwa upasuaji huo Novemba 8, mwaka huu katika
Hospitali ya John Hopkins iliyopo Baltimore, Jimbo la Maryland,
Marekani.Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, mastaa
wamesema wameguswa na kuumwa huko kwa rais lakini wameshukuru kwamba
upasuaji umefanyika salama hivyo wanamuombea apone haraka ili aweze
kurudi katika afya yake ya kawaida.
“Mungu asaidie upone haraka baba…tunaumwa nawe,” aliandika Aman Temba
‘Mh. Temba’ mtandaoni huku Esterlina Sanga ‘Linah’ akiandika:“Furaha ya
moyo wangu inakamilika na mengi lakini kubwa kuliko yote ni kuona
tabasamu lenye afya na uzima tele kwako baba, shujaa rais wangu. Get
well soon my shujaa.”
Mbali na wasanii hao, wengine walioonesha kuguswa na kuumwa kwa rais
na kuandika hisia zao ni Diamond, Linex, Wolper, Shetta, Shilole na
MwanaFa.
Mbali na wasanii wananchi mbalimbali wa kawaida kwa nyakati tofauti walieleza hisia zao kupitia gazeti hili:
“Nilipopata tu taarifa kwamba mheshimiwa rais amefanyiwa upasuaji,
nilishtuka kidogo lakini baada ya hapo mimi pamoja na wenzangu tukafanya
maombi maalumu ya kumuombea rais wetu aweze kupona haraka na kuendelea
na majukumu yake ya kawaida.
“Niwaombe Watanzania wote tuungane kwa pamoja kumuombea rais wetu
maana maombi yetu yana maana kubwa mbele za Mungu,” alisema Mazula,
mkazi wa Tabata.
Tezi dume ni nini?
Tezi dume ipo kwa binadamu wa kiume ambapo ina muonekano kama wa yai
(oval shape) na upana wake huwa ni CM4 na unene CM3 ingawa kwa mujibu wa
madaktari, vipimo hivyo vinatofautiana kwa kila mwanaume.
Tezi dume inazunguka shingo ya kibofu cha mkojo na kuzunguka mrija
unaopeleka mkojo nje, kwa kawaida tezi hii ina umbo la wastani na
huongezeka ukubwa kadri umri wa mtu unavyozidi kuongezeka.
0 maoni:
Post a Comment