BAO pekee la mshambuliaji wa kimataifa wa Italia,
Mario
Balotelli limeipa Liverpool ushindi wa 1-0 dhidi ya Besiktas katika
mchezo wa kwanza hatua ya 32 Bora Europa League Uwanja wa Anfield usiku wa jana.
Mshambuliaji huyo wa
zamani wa Manchester City, Inter Milan na AC Milan, alifunga bao hilo
kwa penalti dakika ya 85, kufuatia winga Jordon Ibe kuchezewa faulo
kwenye eneo la hatari.
Mtaliano huyo alimpokonya mpira Nahodha Jordan Henderson na ‘akazinguana’ na Daniel Sturridge kabla ya kwenda kupiga.
Mapema,
Demba Ba na Adam Lallana walipoteza nafasi nzuri za kufunga kwa kila
timu na baada ya ushindi huo mwembamba Anfield, Liverpool inajiweka
katika mazingira magumu kuelekea mchezo wa marudiano nchini Uturuki
Alhamisi ijayo.
Kikosi cha
Liverpool kilikuwa; Mignolet, Can, Skrtel, Sakho, Ibe, Henderson,
Allen/Lovren dk63, Moreno, Lallana/Sterling dk77, Sturridge na
Coutinho/Balotelli dk63.
Besiktas: Gonen, Kurtulus, Franco, Gulum, Ramon, Hutchinson, Kavlak, Tore, Sosa/Ozyakup dk60, Sahan/Frei dk72 na Ba.
Balotelli akishangilia 'kigumu' mbele ya mashabiki wa Liverpool baada ya kufunga
0 maoni:
Post a Comment