MSHAMBULIAJI wa Mabingwa wa
zamani wa ligi kuu ya Tanzania bara, Dar es salaam Young Africans, Simon
Msuvu baada ya kufanikiwa kuipandisha timu yake katika kilele cha ligi
hiyo kwa kuifungia mabao mawili kati ya matatu katika mchezo dhidi ya
Tanzania Prisons, mshambuliaji huyo amefunguka na kudai kuwa anajisikia
vizuri anapopangwa kucheza na Ngassa au Sherman.
Akizungumza na Shaffihdauda.com
baada ya mchezo huo, Alipoulizw nani kati ya nyota hao wawili
anawakubali akicheza nao, Msuva amesema kuwa yeye ni mchezaji hivyo
haweze kuchagua nani wa kucheza naye lakini akipangwa na yoyote kati ya
Mrisho Ngassa na Khap Sherman lazima atekeleze majukumu yake kama
mchezaji.
“ Ah hiyo ni kazi ya mwalimu,
yeye ndio anajua amuanzishe nani asimuanzishe nani, hayo ni majukumu
yake, Mimi mtu yoyote nitakayepewa nicheze naye nacheza naye” Amesema
Simon Msuva amabye ameibuku shujaa kwa kifumania nyavu mara mbili
akiiteketeza Prisons katika uwanja wao wa Nyumbani Sokoine, Jijini
Mbeya.
Akizungumzia mchezo huo kwa
ujumla Msva amewasifia Prisons kwa kusema kuwa ni timu nzuri lakini
baadhi ya makosa madogo madogo ndio yaliyowagharimu hadi wao kuibuka na
pointi tatu na mabao matatu.
“Prisons ni timu nzuri sio kwamba
ni timu mbovu, sema makosa ambayo wao wliyateda sisi ndio tuliyatumia
na ndio maana tumeweza kutoka na ushindi” Amemalizia Msuva.
Katika mchezo huo Yanga ilipata
bao la kwanza katika dakika ya 3 kupitia kwa Simon Msuva ambaye
aliunganisha kona safi kutoka kwa Mbrazil Andrey Coutinho, Dakika nane
baadaye Beki wa Prisons Lugano Mwagama, akaiandikia Yanga bao lapili
akiwa katika harakati za kuokoa shuti kali lililopigwa na Coutinho na
kumbabatiza na kuingia langoni, hadi dakia 45 za kwanza zinamalizika
Yanga walikuwa wakiongoza kwa bao 2-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa
kasi huku Prisons wakitengeneza nafasi za mapema lakini wakashindwa
kuzitumia, Kunako dakika ya 62 kwa mara nyingine Msuva akaiandikia Yanga
bao la tatu baada ya kuunganisha kona iliyochongwa na Andrey Coutinho
na kufanya hadi dakika 90 zinakatika Yanga 3 Prisons 0.
0 maoni:
Post a Comment