Feb 19, 2015

YANGA YAPAA KILELENI LIGI KUU BARA

Na Prince Akbar, MBEYA
YANGA SC imeweka ‘kishoka’ kiti cha mbele kwenye basi la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji Prisons jioni ya leo Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Yanga SC sasa wanatimiza pointi 28 baada ya kucheza mechi 14, wakiwazidi kwa pointi mbili, mabingwa watetezi, Azam FC ambao jioni ya leo wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Ruvu Shooting. 
Winga Simon Msuva alifunga mabao mawili katika ushindi huo, wakati bao lingine Prisosn walijifunga wenyewe.
Lakini sifa zimuendee kiungo Mbrazil, aliyepika mabao yote matatu jioni ya leo Uwanja wa Sokoine.
Simon Msuva kulia amefunga mabao mawili

Coutinho anayecheza pembeni pande zote mbili, alipiga kona nzuri dakika ya tatu ikaunganishwa nyavuni na Msuva kabla ya kupiga shuti kali dakika ya 11 ambalo beki wa Prisons, Lugano alijifunga katika harakati za kuokoa.  
Coutinho tena, alipiga kona nzuri kumsetia Msuva kufunga bao la tatu dakika ya 62. 
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Kevin Yondan/Rajab Zahir dk78, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite/Salum Telela dk54, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amisi Tambwe, Mrisho Ngassa na Andrey Coutinho/Danny Mrwanda dk66.
Prisons; Mohammed Yussuf, Salum Kimenya, Laurian Mpalile, James Mwasote, Nurdin Chona, Lugano Mwangama, Jeremiah Juma, Freddy Chudu, Jacob Mwakalobo, Amir Omar na Boniface Hau.

0 maoni:

Post a Comment