Feb 19, 2015

AZAM FC YABANWA NA RUVU, SARE 0-0 MABATINI

Na Princess Asia, MLANDIZI
RUVU Shooting imewapunguza kasi mabingwa watetezi Azam FC, baada ya kuwalazimisha sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni hii Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Matokeo hayo yanaifanya Azam FC ifikishe pointi 26 baada ya kucheza mechi 14, hivyo kuangukia nafasi ya pili, Yanga SC ikipanda kileleni baada ya kufikisha pointi 28, kufuatia ushindi wao wa eo dhidi ya Prisons mjini Mbeya.
Hata hivyo, Azam FC itabidi wajilaumu wenyewe kwa sare hiyo, kwani walipata nafasi kadhaa za kufunga mabao wakashindwa kuzitumia.

Dakika ya 26 Kipre Tchetche alipata nafasi nzuri, lakini akapiga nje, kabla ya John Bocco naye kushindwa kumalizia kazi nzuri ya Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dakika ya 35.
Bocco tena alichelewa kuifikia krosi nzuri ya beki Shomary Kapombe aliyepanda kusaidia mashambulizi. Bocco tena dakika ya 62 akashindwa kumalizia pasi ya Himid Mao.
Ruvu Shooting nao walipata nafasi mbili japokuwa hazikuwa nzuri kama za Azam FC dakika ya 37 wakati kipa Aishi Manula alipodaka shuti la Yahya Tumbo. 
Dakika ya 83 pia, shuti la Abdulrahman Abdulrahman lilipanguliwa na kipa bora chipukizi Tanzania, Aishi Manula baada ya pasi ya Tumbo. 
Kikosi cha Ruvu Shooting kilikuwa; Abdallah Abdallah, Michael Pius, Said Madega, Hamisi Kasanga, Frank Msese, Kassim Dabbi, Juma Nade/Bakari Miawi dk63, Hamisi Maulid/Justin Chagula dk63, Yahya Tumbo, Juma Nampaka na Abdulrahman Abdulramhan. 
Azam FC; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, Said Mourad, Serge Wawa, Mudathir Yahya, Himid Mao, Frank Domayo/Didier Kavumbangu dk60, John Bocco, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Kipre Tchetche. 

0 maoni:

Post a Comment