REAL
Madrid imebisha hodi robo Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya, kufuatia
ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Schalke nchini Ujerumani.
Cristiano
Ronaldo aliifungia bao la kuongoza timu ya Carlos Ancelotti dakika ya
25 kwa kichwa na kumaliza ukame wa mabao uliodumu kwa karibu saa tano
upande wake. Kwa Ronaldo hilo linakuwa bao lake la 58 Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa timu yake Real Madrid.
Marcelo akaifungia Real Madrid bao la pili dakika ya 78 na kuihakikishia timu yake ushindi mzuri wa ugenini.
Kikosi
cha Real Madrid kilikuwa; Casillas, Marcelo, Pepe, Varane,
Carvajal/Arbeloa dk81, Silva, Kroos, Isco/Illarramendi dk84, Bale,
Benzema/Hernandez dk78 na Ronaldo.
Schalke:
Wellenreuther, Uchida, Howedes, Matip, Nastasic, Aogo,
Neustadter/Kirchoff dk56, Hoger/Meye dk81, Boateng, Choupo-Moting na
Huntelaar/Platte dk32.
Cristiano
Ronaldo amefunga bao lake la 58 Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa timu yake
Real Madrid ikishinda 2-0 dhidi ya Schalke usiku huu
0 maoni:
Post a Comment