KOCHA mkuu wa Yanga Hans van der Pluijm amesema kwamba Nahodha
wake, Nadir Haroub 'Cannavaro' yuko kwenye hatihati ya kucheza mechi ya
kwanza ya Raundi ya Awali, Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya BDF XI ya
Botswana Jumamosi.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo Dar es Salaam, Pluijm amesema ukiacha shaka hiyo juu ya Cannavaro, kila kitu kuhusu timu yake kipo sawa ambapo anazidi kufurahia umoja, mshikamano na utulivu waliokuwa nao vijana wake.
Pluijm amesema wapo tayari kwa kila kitu kuhusu wapinzani wao hao, lakini hofu yao ni maumivu aliyokuwa nayo Cannavaro ambaye goti lake la kulia.
"Hatujajua kama atakuwa sawa mpaka siku ya mchezo ni jambo la kusubiria leo na kesho kuangalia maendeleo yake lakini tunaimani atakuwa sawa, mbali na hapo naweza kusema tupo tayari kuingia vitani kupambana na hao Wanajeshi,"amesema Pluijm.
Wakati huo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Yanga Jerry Muro amesema tayari wameanza kuuza tiketi za mchezo huo dhidi ya BDF ambao wanatua leo jioni na ndege maalum ya jeshi la Botswana.
"Wapinzani wetu wanaingia leo na ndege maalum ya jeshi la kwao na waankuja na msafara qwa wachezaji 25 pamoja na viongozi wao tunaomba wale wote wanaoipenda Yanga kununua tiketi mapema kuanzia leo ili kupunguza msongamano siku ya mchezo na siku hiyo milango ya Uwanja itafunguliwa mapema kuanzia saa saba mchana,"alisema Murro.

0 maoni:
Post a Comment