KOCHA
Mkuu wa Simba Mserbia, Goran Kopunovic, amewataka wachezaji wa timu
hiyo kutojikuza na badala yake wanatakiwa kupambana na kujituma kwa
lengo la kushinda mechi za ligi ili wapate mafanikio.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini Morogoro Kopunovic alisema juhudi na kila mchezaji kufahamu majukumu yake ndiyo silaha pekee itakayowapa mafanikio na hatimaye kutimiza ndoto.
Alisema kuwa anawakumbusha wachezaji wake kutoidharau timu yoyote katika ligi hiyo ambayo mechi zote wanazocheza zina ushindani.
" Ligi ni ngumu na ina ushindani, nawaeleza mara kwa mara wajitume na wajue kwamba wao bado wako chini na hakuna anayepaswa kujiona ni bora", alisema Kopunovic.
Kocha huyo naye aliungana na Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van der Pluijm, kuuponda Uwanja wa Jamhuri kuwa hauna ubora na unasumbua wachezaji wake kucheza soka la kuburudisha.
Kopunovic pia aliuponda uwanja wa Mkwakwani Tanga kuwa unafanya wachezaji wacheze kulingana na miundombinu ya uwanja huo na si vile walivyofundishwa.
Simba iko mkoani Morogoro tangu jana kwa ajili ya mechi yao ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Polisi Morogoro ambayo inatarajiwa kufanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani humo.
Wenyeji Polisi Morogoro wanaofundishwa na Adolph Rishard watashuka dimbani wakiwa na pointi 18 wakati Simba wana pointi 17.

Kocha wa Simba SC, Goran Kopunovic kushoto akiwa na wachezaji wake |

0 maoni:
Post a Comment