BAO
la dakika za lala salama la Willian, limeipa Chelsea ushindi wa 1-0
dhidi ya Everton usiku huu katika mcheo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa
Stamford Bridge, London.
Toffees
walifungwa bao hilo baada ya kumpoteza mchezaji wake, Gareth Barry
aliyetolewa kwa kadi nyekundu na sasa The Blues wanaendelea kuongoza
Ligi Kuu kwa pointi saba zaidi.
Steven
Naismith alikuwa mwenye bahati baada ya kuepuka adhabu licha ya kuunawa
mpira kwenye boksi la Everton kipindi cha kwanza.
Kiungo
mpya, Juan Cuadrado alianza kwa amra ya kwanza leo tangu asajiliwe kwa
Pauni Milioni 27 Chelsea kutoka Fiorentina na akavutia.
Willian akishangilia na Didier Drogba baada ya kufunga
0 maoni:
Post a Comment