Kuna time utakuwa unajiuliza maswali kuwa kuna umuhimu gani kwa wasanii wa hapa Tanzania kufanya kolabo na mastaa wa Afrika .
Sasa staa wa Bongo Fleva Ali Kiba amejibu swali lako na kusema;‘Katika
kutangaza muziki inasaidia kiasi fulani lakini sio sana, muziki unaweza
ukautangaza hata wewe mwenyewe, mimi binafsi muziki wangu nimeutangaza
mbali sidhani kama Afrika hainijui bali inanifahamu sema tu kiukweli
video zangu nilizokuwa nafanya hazikuwa katika quality nzuri huo ni
ukweli naujua kwa hiyo sasa hivi tuko vizuri katika kujipanga
nahakikisha kila kitu kitakuwa poa, hiyo inasaidia sana vile vile
kubadilisha muziki na kuutangaza muziki wako katika msanii yoyote
ambaye umemchukua labda wa Congo, Nigeria, Uganda, sehemu nyingine
nyingi ili watu waweza kukusikiliza kwa urahisi na vile vile ni
support kubwa inaonesha jinsi gani una ushirikiano na watu wengine‘-Alisema.
0 maoni:
Post a Comment