MABINGWA
watetezi wa Ligi Kuu ya England, Manchester City wameibuka leo na
kushinda mabao 4-1 dhidi ya Stoke Uwanja wa Britannia huo ukiwa ushindi
wa kwanza tangu mwaka mpya.
Sergio
Aguero aliwafungia wageni bao la kwanza dakika ya 33, kabla ya Peter
Crouch kuisawazishia timu ya Mark Hughes dakika ya 38, hilo likiwa bao
lake la sita msimu huu.
City
ikapata bao la pili dakika ya 10 kipindi cha pili kupitia kwa James
Milner, kabla ya Aguero kufunga la tatu kwa penalti dakika ya 55 na
Samir Nasri la nne dakika ya 76.
Kiungo, Nasri akishangilia baada ya kuifungia Man City bao la nne
0 maoni:
Post a Comment