Kocha wa Yanga, Hans van
der Pluijm amesema watakuwa wakichanganya mazoezi yao katika viwanja vya Karume
na Taifa jijini Dar.
Yanga imeanza rasmi
kujiwinda kwa ajili ya mechi yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya BDF XI ya
Botswana itakayopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Pluijm amesema wameamua
kufanya hivyo kwa malengo tofauti kwa kuwa Taifa ndiyo watakaochezea mechi dhidi ya Waswana nao lakini
Karume itawasaidia kumiliki mpira.
“Eneo la kuchezea na Karume
ni bora zaidi, tukicheza pale ni lahisi wachezaji kupata mazoezi ya kutosha
hasa katika suala la kumiliki mpira.
“Unapocheza nyumbani,
lakini uwe na uhakika wa kukaa na mpira muda mwingi. Hauwezi kushambulia kama
hauna mpira.
0 maoni:
Post a Comment