TIMU
ya Barcelona imeifunga mabao 3-1 Villarreal katika Nusu Fainali ya
kwanza ya Kombe la Mfalme, maarufu Copa del Rey usiku huu Uwanja wa Nou
Camp.
Ushindi huo wa 10
mfululizo katika mashindano yote kwa vigogo hao wa Hispania ulitokana na
mabao ya Lionel Messi, Andres Iniesta na Gerard Pique.
Mwanasoka
Bora wa zamani wa dunia, Muargentina Messi alifunga bao la kwanza
dakika ya 41, kabla ya Villarreal kusawazisha kupitia kwa Manu Trigueros
dakika ya 48.
Andres
Iniesta akaifungia Barcelona bao la pili dakika tatu baadaye kabla ya
Gerard Pique kukamilisha ushindi wa 3-1 dakika ya 65.
Kikosi
cha Barcelona kilikuwa: Ter Stegen, Alves, Pique, Mathieu, Alba,
Rafinha/Rakitic dk69, Mascherano, Iniesta, Messi, Suarez na Neymar.
Villarreal:
Asenjo, Mario, Musacchio, Victor Ruiz, Costa, Jonathan dos Santos,
Pina, Bruno/Trigueros dk33, Cheryshev/Gomez dk74, Giovani dos
Santos/Rukavina dk52 na Vietto.
Wachezaji wa Barcelona wakifurahia ushindi wao dhidi ya Villarreal Uwanja wa Nou Camp katika Nusu Fainali ya Copa del Rey.
0 maoni:
Post a Comment