Kocha Goran Kopunovic amesema kiungo wake Saidi
Ndemla atakuwa fiti kabla ya kuivaa Polisi Moro.
Simba ina kibarua Jumapili dhidi ya timu hiyo
ngumu kutoka mkoani Morogoro.
Kopunovic amesema kwa kuwa Ndemla ameanza
mazoezi kwa zaidi ya siku tatu sasa, anaamini atakuwa fiti.
“Atakuwa fiti hasa kama hakutakuwa na tatizo
hapa katikati. Kurejea kwake kunafanya kwue na upana wa uchaguzi.
“Timu inapokuwa na majeruhi wengi ni tatizo kwa kocha, uchaguzi wa nani umtumie au fomesheni ipi uchague linakuwa tatizo,” alisema Kopunovic.
0 maoni:
Post a Comment